Menu

01. Mkutano wa mhariri, waandishi wa habari na habari zitakazo rushwa

Uwandishi wa habari ni kazi inayohitaji uwepo wa mshikamano wa timu. Watangazaji wanahitaji kujua kile maripota watakacho leta. Maripota wanaitaji kujua ni mada zipi habari imechagua kueleza tukio. Mhariri mkuu anahitaji kuwatia moyo wanatimu yake na kuratibu kazi ya habari. Mkutano wa mhariri, waandishi wa habari na habari zitakazo rushwa ni wakati wote wanakutana na sehemu ambapo kwa pamoja mada za siku zina chaguliwa.

Redio zina mikutano mitatu kwa siku.

Ile ya asubui ni mkutano mkuu ambayo imepangwa saa tatu asubui, baada ya habari za asubui, ambapo mada za siku zinajulikana. Mkutano mwingine ni nida ya mchana kwa ajili ya kuendeleza habari kuu za siku zinazoendelea. Mkutano wa mwisho ni jioni baada ya habari za mwisho wa siku na kabla za habari za usiku, ambapo mambo muhimu yanakusanywa na kuandaa habari muhimu za kesho yake asubui.

Mkutano wa mhariri, wandishi wa habari na habari zitakazo rushwa una muda mdogo.

Washiriki wa mkutano wana nidhamu na wanajiheshimu. Sio sebuleni ambapo tunazungumza kitu chochote kile. Mkutano una dakika 45 ili marepota waweze kuondoka haraka iwezekanavyo kutafuta habari nje na kuwaachia watangazaji kuandaa habari yao.

Mbinu za kuongoza mkutano.

Kwanza, kiongozi ni mhariri mkuu, anakuja na orodha za mada na anazigawa kwa wanatimu wote.
Pili, uwendeshaji wa kisasa. Waandishi wa habari wanatoa mawazo yao, mitazamo yao juu matukio mbali mbali, na kuchagua mada muhimu: Mihadi zimeshachukuliwa, mkutano kwa waandishi wa habari, uchunguzi unaoendelea.

Mfano: Mkutano wa asubui.

Saa tatu kamili, waandishi wote wa habari wanapaswa kuhudhuria mkutano. Muda uzingatiwa.

Hatua ya kwanza:

Watangazaji wa asubui wanapewa nafasi ya kuzungumza kwanza kwa ajili ya uchambuzi wa uwakika wa mada mbali mbali: ripoti zilikuwa za kuridhisha, kuna kitu chochote tulicho kosa, jinsi gani tutakavyo pata kile tulichokosa…?

Waandishi wa habari na mhariri mkuu wanapewa nafasi ya kuongea baada ya watangazji wa asubui kwa ajili ya uchambuzi wa haraka haraka.

Yote ndani ya dakika kumi bila mvutano na mambo yasiyokuwa ya msingi.

Hatua ya pili:

Zamu kwa kila dawati: mawazo ya waandishi wa habari na maoni yao juu za habari kuu za siku. Kizuri ni kuwa na ubao mkubwa mweupe unaoweza kufutika, ambapo tunaweka dondoo muhimu ngazi kwa ngazi, na hapo kila mtu anaweza kuona.

Kukabiliana na ajenda ya siku, kuangalia yale muhimu, yale tutakayoendeleza baadaye.

Dondoo ya mwisho, ndefu kuliko yote, tunachagua na kuzungumza mada mbali mbali yale yatakayo fanyiwa kazi na vipi (ripoti kwa ufupi, sauti, ripoti kamili, wageni…)

Orodha hii ikiwa imekamilika, kila mtu atakuwa ana picha kamili ya yale yatakayofanyika. Majadiliano, ushirikiano unawezesha kuendeleza ufanisi wa timu.

Mikutano mengine miwili ya mhariri, wandishi wa habari na habari zitakazo rushwa, mchana na jioni, ni marudio tu ya yale yaliyozungumzwa asubui.