Menu

18. Kanuni kuu za HTML

Kwa intaneti HTML ni sawa na alfabeti kwa maandishi: ni seti ya herufi zinazotoa viashiria vya maana ya maudhui na mantiki mahsusi ya uainishaji wa maudhui. Kwa hiyo msimbo huo ni muhimu sana kwa kuboresha urejeaji wa habari.

Fasili ya msimbo wa HTML

Msimbo wa HTML ni aina ya lugha ya kutafsiri lugha nyingine inayoonesha viashiria vya namna ya utendaji wa maudhui ya habari. Unaundwa na “tags”, “tag” ya kwanza inayoainisha mpangilio utakaotumika na “tag” ya mwisho inayoonesha mwisho wa mpangilio. Kwa mfano, kiungo kilichowekwa kwenye habari kinafasiliwa na “tag” hii:

<a href= »XXXX XXXXXX » target= »_blank »>XXXXXXX XXXXXXX</a>

Sehemu ya kwanza inaonesha anwani ya URL (href, rejea) ambayo kwayo neno linalobonyezeka (target blank, lengo) litakupeleka.

“Tags” kuu za kuzijua

“Tags” kadhaa zinaonesha misimbo muhimu ya maandishi:

<strong> au <b> (bold) inaonesha neno lililokolezwa wino

<i> au <em> inaonesha neno lililolazwa

<p> inaonesha mwanzo wa aya na </p> inaonesha mwisho wake, ikiwa na jongezo katika mstari wa aya hiyo.

<center> hukuwezesha kuweka maandishi au picha katikati ya skrini

“Tag” hii hukuwezesha kuweka picha ya muundo wa .jpg pamoja na maelezo yake:

<img src= »/files/XXXX XXXXX.jpg » title= »CREDIT » alt= »CREDIT »>

“Tags” nyingine ngumu zaidi zinakuwezesha kuweka sauti, picha na video. Kwa mfano, msimbo ambayo majukwaa ya kushirikisha maudhui hukuwezesha kunakili na kubandika kwenye maudhui yako pia ni “tag” ya HTML.