Menu

08. ukweli … wingi

Kuhabarisha ni kutoa habari. Habari inayotolewa lazima iwe kwa ufupi. Kama habari haiko kwa ufupi, si habari tena; ni uongo. Habari ni kuweka maelezo yaliyotolewa katika maneno. Ikiwa habari hiyo inaandikwa kwa namna ambayo inapotosha maudhui yake, huo ni upotoshaji. Jukumu kuu la mwandishi wa habari msomi ni kutimiliza haki ya umma ya kupata habari sahihi.

UKWELI LAZIMA UHESHIMIKE

Ili kuheshimu ukweli, lazima kupima uhalisia wa huo ukweli kwa umakini sana. Ukweli unaoonekana unaweza kuwa umepotoka, hata kama unauona kwa macho yako mwenyewe. Ni muhimu kuchukua muda kuelewa unachokiona ili kuhakikisha kwamba hutoi tafsiri potofu ya maana halisi ya ukweli unaouona.
Mfano: Namuona mtu akimpiga mtu mwingine mtaani. Kinachoonekana kinaelekea kuwa dhahiri: Namwona mpigaji na mpigwaji. Lakini kuna jambo lingine hapa linaloendelea ambalo silioni?

MCHAKATO WA UTAMBUAJI

Kuna utaratibu wa kitaalamu unaopaswa kufuatwa ili kubaini ukweli wa kile tunachokiona na kukiandikwa kiukweli kadri iwezekanavyo.

Unapokuwa unashuhudia jambo moja kwa moja:

  • Zingatia kwamba unaona sehemu tu ya ukweli,
  • Hoji maana halisi ya usichokijua kwa kile unachokiona,
  • Linganisha ufahamu wako na ule wa mashuhuda wengine (“Je, uliona nilichokiona? Sina uhakika kama niliona sawa sawa: wewe uliona nini?”),
  • Pangilia matukio katika mtiririko wa kutokea kwake,
  • Weka matukio hayo katika muktadha,
  • Andika ukweli bila ya upendeleo, kufupisha au kutoa tafsiri yako.
  • Acha habari yako isomwe na mwenzako kuhakikisha kwamba maudhi hayapotoshi.

Unapokua hushuhudii jambo moja kwa moja:

  • Thibitisha ni kwa kiasi gani maelezo ya mashuhuda yanaweza kuwa ya kutegemewa,
  • Hakiki madai yaliyotolewa na mashuhuda,
  • Uliza maafisa maoni yao,
  • Andika habari yako kwa tahadhari: “Kulingana na polisi…”, “Kulingana na shuhuda…”.

UKWELI LAZIMA UTAFUTWE

Pale maslahi binafsi au ya kijamii yanapoingilia juhudi za kupata ukweli, mwandishi wa habari anatawaliwa na wajibu wa kijamii wa kuutafuta ukweli huo. Hata hivyo, utafutaji wa ukweli hauhalalishi matumizi ya mbinu chafu zilizopo. Kuheshimu faragha na utu wa mtu ni vigezo muhimu ambavyo lazima waandishi wa habari wasomi wavifuate. Aidha, katika mambo yahusuyo maslahi ya umma, kutafuta uweli ni lengo halali kabisa, lakini waandishi wa habari si polisi wala mahakimu, kwa hiyo uwezo wao wa kuchunguza una ukomo. Lazima watambue na kulikubali hilo.

Kila wakati mtu fulani anapokuzuia kwa makusudi kutafuta ukweli, epuka ufichaji huo kwa kuwa muwazi.

  • Omba maelezo kwa maandishi.
  • Waeleze wasomaji wako ugumu unaopitia.
  • Tunza shajara inayoelezea utafiti wako.
  • Hifadhi ushahidi kwamba unatenda hivyo kwa nia njema.
  • Sahihisha makosa yako.
  • Kubali makosa yako.

USIWE KING’ANG’ANIZI

Wakati mwingine, kutafuta ukweli inaweza kuwa uraibu kwa mwandishi wa habari, hasa pale anapokutana na vizingiti vingi katika kazi yake. Shauku ya kutafuta ukweli inaweza kusababisha hatari ya wewe mwenyewe kupotosha ukweli huo kutokana na kile utakachokifichua kwenda kinyume na matarajio ya wasomaji. Hatari ya jambo hili ni kubwa zaidi pale mwandishi wa habari anapoweka kando wajibu wake wa kutofungamana na upande wowote kwa kutaka kuhakiki dhana: Ikiwa mwandishi wa habari ataondoa ukweli aliougundua kwa sababu hauendani na nadharia yake, mwandishi wa habari atakuwa hatendi kwa uadilifu.. Hakuna ukweli usiopingika.