Menu

12. trivia

Jambo linalozua mjadala mara kwa mara ni nafasi kiasi gani itengwe kwa ajili ya habari zinazogusa jamii. Kwa kawaida huwa zinaenda kinyume na msimamo wa vyombo vya habari na maoni ya wadau wao wasomi. Lakini jibu ni dhahiri. Habari zinazogusa jamii ni sehemu ya maisha ya kila siku, ni za uhalisia sawa sawa na habari zinazoandika siasa, biashara, jamii au utamaduni. “Msema ukweli” hawezi kupuuza uhalisia wa habari hizi katika maisha ambazo hutoa majibu ya papo hapo. Jambo muhimu ni kujua namna gani ya kuziandika.

HABARI ZINAZOGUSA JAMII ZINAONESHA UHALISIA WA MAISHA KATIKA JAMII.

Damu, machozi na majonzi ndiyo vipengele muhimu vya habari zinazogusa jamii na daima zina mguso wa kihisia. Zinahitaji kuandikwa kwa umakini zaidi kuliko hata habari nyingine.

KOSA DOGO TU KATIKA MAELEZO YA KINA LINAWEZA KUWA NA MADHARA MAKUBWA KABISA KWA WANAOHUSIKA.

  • Pambanua vyanzo vya habari vya kuaminika: polisi na askari wa zimamoto, watoa huduma ya kwanza, watoa msaada wa kwanza wa kitiba na wafanyakazi wengine wa hospitali.
  • Panga kuwa na kikao cha kila siku na wafanyakazi ambao ni rahisi zaidi kuwafikia.
  • Thibitisha upya maelezo unayopewa kwa kutumia chanzo kingine cha habari.
  • Waombe mashuhuda wowote waliopo maoni yao.
  • Elezea tu ukweli uliothibitika.
  • Epuka upendeleo.
  • Ripoti taarifa rasmi bila upendeleo. Hata kama itakuwa imeripotiwa kwa maandishi, hutaandika: “Gari lilipitiliza kwenye taa nyekundu na kumgonga mwenda kwa miguu.” Badala yake utatumia lugha ya sintofahamu na kuelezea bila kuegemea kokote kuandika: “Mwenda kwa miguu aligongwa na gari na kufa ambalo inasemekana lilipitiliza kwenye taa nyekundu, kulingana na taarifa zizliotolewa na mashuhuda na polisi… 

KILA MTU ANAWEZA KUGUSWA NA HABARI ZINAZOGUSA JAMII.

Habari zinazogusa jamii ni matokeo ya ghafla ambayo yana ukaribu na kila mtu kwa kila maana ya neno hilo, kulingana na muda, mahali na hisia. Kila mtu anaweza kuguswa na habari hizi kwa vile zinaweza kutokea kwa mtu yeyote, mahali popote, kwa wakati wowote. Mguso wa kihisia wa habari hizi lazima uzingatiwe wakati wa kuziandika.

UTU WA MTU NA FARAGHA LAZIMA KUHESHIMIWA.

Kuheshimu haki ya kuwa na faragha na utu wa mtu ni sehemu ya maadili makuu ambayo waandishi wa habari lazima wayafate. kwa hiyo waandishi wa habari lazima waendelee kutokuwa na upendeleo wanapoandika habari zinazogusa jamii za watu wa kawaida na kuweka uwiano kati ya haki ya umma ya kupata habari na haki ya mtu binafsi ya kuwa na faragha pale habari zinazogusa jamii zinapohusu watu maarufu katika jamii.

MASHARTI 7

  1. Tunza siri ya watu wote binafsi wanaohusishwa katika habari inayogusa jamii. Unaweza kuleta kizaazaa kwa kumtaja tu mtu kwa jina katika habari yako au kwa bahati mbaya kufichua maelezo fulani kidogo. Unaweza kusababisha madhara makubwa na ya kudumu kwa kunukuliwa tu hadharani kama sehemu ya uchunguzi wa polisi au wa mahakama.
  2. Usitoe nambari ya usajili wa gari ya gari lolote lililohusika katika ajali ya barabarani.
  3. Usitoe maelezo yoyote ya kina kuhusu maisha binafsi ya mtu, hasa pale inapohusu kujiua.
  4. Epuka kuandika maelezo yoyote ya kina kuhusu makosa ya ngono yaliyotendeka kwa vile haina maana kuelezea mambo ya utupu.
  5. Kamwe usijibu maswali yanayouliza “Nani? Nini?” na “Namna gani?” kwa kutoa maelezo yanayoweza kumhusisha katika kosa mtu fulani. 
  6. Epuka kutafsiri maana ya maelezo kwa vile unaweza kuvuruga ukweli. Hutaandika: “Dereva mlevi mweusi…” au “Dereva mlevi mzungu…”. Badala yake utaandika tu: “Dereva mlevi…” kwa sababu mwonekano wa dereva au tabia yake haina uhusiano na uwezo wake wa kuendesha.
  7. Chukulia kwamba kila mtu hana hatia hadi itakapothibitishwa na mahakama. Bila kujali kwamba ni mtu mashuhuri au la, mtu yeyote anayehusishwa katika habari inayogusa jamii ana haki ya kutunziwa utu wake na tabia, hata kama watakuwa wanachukuliwa kwamba ni watuhumiwa na mamlaka husika.

KADRI MIHEMKO INAVYOKUWA JUU, NDIVYO PIA UANDISHI WAKO USIEGEMEE UPANDE WOWOTE

Iwe habari yako inayogusa jamii inaongelea majanga ya kiasili au makosa ya jinai, uandishi wako haupaswi kuchochea hisa kali zilizopo tayari ambazo habari hizi husababisha. Unapaswa kuwa na staha wakati wa kuziandika na kuepuka kutumia vivumishi (kama vile “kufisha”, “janga”, “kushangaza” au “kutisha”).

MANENO SAHIHI KWA MADA NYETI

Uandishi wa habari usio na upendeleo unataka matumizi ya maneno sahihi kwa kila tukio. Ingawa “mauaji yote ya binadamu” ni “mauaji”, lakini si kila “mauaji” ni “mauaji ya binadamu”. Mauaji ya binadamu yanataka uthibitisho wa nia ovu ya kabla ili kuthibitisha kosa la mauaji.

Maauji bila kukusudia ni tendo la kumuua mtu, lakini inaweza kuwa ama kwa kukusudia au kutokukusudia. “Shahidi” si “mshtakiwa”. “Mhutumiwa” si lazima awe “na hatia”. Na kuna tofauti kati ya “mtu anayechukuliwa kama mkosaji” na mtu ambaye “ametiwa hatiani”. Mwandishi yeyote wa habari anayeandika habari zinazogusa jamii lazima awe na uelewa wa lugha ya kisheria ili aweze kutumia maneno sahihi pale anapoandika habari ambazo madhara yasiyoweza kusahihishwa   yanaweza kutokea kwa kutumia neno lisilo sahihi, hata kama litaonekana ni kwa nia njema tu.

MWELEKEO WA KIJAMII

Habari zinazogusa jamii huhusu maadili mazito katika maisha ya kila siku kama vile mapenzi, chuki, urafiki, usaliti, uaminifu na kuvunja uaminifu. Ni dirisha la kuiangazia dunia na huakisi dhana za kidunia. Baadhi ya habari hizo huwa maarufu kuliko nyingine kwa sababu zina mguso kwa jamii. Zinakuwa “mwelekeo wa kijamii”. Mama wa familia maskini anayeiba mkate kutoka dukani ili akawalishe watoto wake ni zaidi ya kosa la wizi – ni dirisha la kuangazia hali ya sasa ya ubinadamu. Kama kijana asiye na kazi akijiua Ulaya kama kitendo cha kulalamikia hali hiyo, inaweza kuwa chanzo cha mapinduzi katika siku za usoni… Kwa kuwa mwelekeo wa kijamii, habari inayogusa jamii inakuwa habari inayostahili kuandikwa kwenye ripoti au habari za uchunguzi.

Walakini, kuwa makini! Habari kuu zinapaswa kuandikwa bila ya kutumia lugha ya kishabiki. Kadri habari inavyokuwa motomoto, ndivyo ilivyo muhimu kwa mwandishi wa habari adumu kuwa muungwana.