Menu

02. Misemo ya kiufundi ya mwandishi wa habari wa redio

Bila shaka mwandishi wa habari anapaswa kujua kutumia baadhi ya masuala ya kiufundi ili aweze kufanya kazi yake. Lakini kuwa mzuri kwenye mahojiano na uwandishi haitoshi. Inabidi uweze kuweka kazi yako kwenye ile ya timu nzima. Ndio hii wanacho kiita kuchangia tamaduni za kitaalamu.

Kuchangia tamaduni za kitaalamu ni kuzungumza lugha moja.

Hapa chini baadhi ya misamiati muhimu.

Utagulizi wa ripoti: nakala inayosomwa na mtangazaji wa habari kwa ajili ya kutoa utangulizi juu ya ripoti inaitwa pia intro.

Hitimisho ya habari: Nakala inayosomwa na mtangazaji baada ya kurusha ripoti na inahitimisha mada inaitwa pia outro.

Attaque : Mwanzo wa mada.

Chute : Mwisho wa mada.

Kifungua habari: Habari ya kwanza.

Kifungua habari batili: Ni msemo unaotumika wakati habari ya kwanza haijakidhi lengo la kichwa cha habari.

Habari kwa ufupi: Ni habari isiokuwa kamili, yaani, kwa lugha nyingine, dondoo…

Habari kwa ufupi: Ni ripoti kutoka mwandishi wa habari hisiyo kuwa na mahojiano.

Sauti: Ripoti iliyo na muundo wa mahojiano.

Ripoti kamili: Ni ripoti inayojumuhisha habari kwa ufupi na sauti za mahojiano

Mwongozo wa habari: Ni hati iliyoandikwa na mtangazaji ili kumwezesha fundi mitambo kurusha habari.

Maneno hayo ni mifano tu. Kwa watu wengi maneno hayo hayaeleweki. Kwa timu ya redio ni maneno ya kila siku, msamiati huu unaochangiwa na wote ni ishara ya tamaduni moja na inayofanana.

Kuzingatia taratibu

Kuchangia tamaduni ya kitaalamu ni vile vile kuheshimu taratibu zinazofanana na zinazowezesha kazi ya kila mwandishi wa habari kujiandikisha kwenye utayarishaji wa vipindi vya redio.

Mfano: Hebu tufikirie mwandishi wa habari anayeacha ripoti yake popote pale au kwenye mtandao wa kompyuta wa redio na sio kwenye faili iliyopo kwa ajili ya kuchangia habari. Mwandishi huyo wa habari anarudi nyumbani kwake huku akiwa ana uwakika amekamilisha ripoti yake, wenzake wanaoandaa habari kesho yake asubui watapoteza muda kutafuta ripoti ile.Kama ripota angeheshimu taratibu angesaidia muda husipotee na wenzake wasiwe na wasi wasi.

Kama kuna shaka yoyote inabidi kurejea kwa uongozi.

Wakati mwingine mshirika anapaswa kukabiliana na hali ya kipekee. Hajui uwamuzi ngani kufanya. Kwa hali hiyo, husisite kutoa tatizo lako kwa mkuu wako.